Alhamisi , 26th Oct , 2023

Jeshi la Israel (IDF) limefanya "uvamizi uliolenga eneo la adui " usiku wa kuamkia leo kaskazini mwa Gaza kwa kutumia vifaru.

Israel haijaanzisha uvamizi wake wa ardhini katika Ukanda wa Gaza - lakini inasema uvamizi huo ulikuwa katika "maandalizi ya hatua zijazo za mapambano".

Wakati Israel ikisema mashambulizi yake ya anga yalilenga maeneo 250 ya Hamas katika kipindi cha saa 24 zilizopita, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema hakuna mahali salama Gaza.

Wizara ya afya ya Hamas katika Ukanda wa Gaza inasema karibu watu 6,500 wameuawa tangu Oktoba 7 mwaka huu.

Zaidi ya watu 1,400 waliuawa katika mashambulizi ya awali dhidi ya Israel yaliyofanywa na kundi la Hamas, na zaidi ya watu 200 bado wanashikiliwa mateka Gaza.

 

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa onyo kuhusu kuongezeka kwa mzozo wa mafuta Gaza.

 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowakilisha Wapalestina katika Ukanda wa Gaza limesema limepata mafuta ambayo yatapewa kipaumbele kwa kuchuja na kusafisha maji