
Akizungumza katika hotuba yake kwa hadhara iliyohudhuria hafla ya ufunguzi wa jengo hilo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiomba PAPU kuyafanya Mashirika ya Posta Barani Afrika yaongeze wigo na ufanisi wa usafirishaji kwa kutumia Mashirika ya Ndege ya Ndani ya Afrika.
“Hali ilivyo sasa hivi ukitaka kwenda West Africa ni hadi uende Europe kwanza halafu uchukue connection uende West Africa, sasa Posta itulazimishe lazima ndege zetu zisafiri ndani ya Afrika kupeleka vifurushi na kusafirisha Watu”
"Tunaomba PAPU ifanye mashirika ya Posta Afrika yaweze kuongeza wigo wa wa ufanisi wa usafirishaji kwa kutumia mashirika ya ndegeya ndani badala ya kutumia mashirika ya nje ya Afrika. Na hii itatulazimisha sasa tuwe na connection ndani ya bara la Afrika" amesisitiza Rais Dkt. Samia.
Katika hatua nyingine Rais Dkt. Samia amesema Umoja wa Posta Afrika unaweza kuleta mageuzi makubwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya bara la Afrika huku akibainisha kuwa kama Posta iliweza kufanya kazi ya kuleta uhuru na basi hata sasa inaweza kuleta mabadiliko ya kidigitali katika huduma za posta ndani ya bara la Africa.
"Posta za Afrika ziweze kuwa na mfumo mmoja utakaowezesha kufanyika kwa biashara matandao kwani tayari takribani kila posta imeanzisha maduka mtandao kuwarahisishia wafanyabiashara shughuli zao, ni imani yangu kuwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefanikiwa kufikia maono ya umoja wa posta Duniani"