Jumatano , 25th Jun , 2014

Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (TAMISEMI) imetoa wito kwa jamii kushiriki kulinda haki za watoto.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa, Kassim Majaliwa.

Ushirikiano huo ni pamoja na serikali na wadau hao kuhakikisha watoto wanakuwa katika mazingira salama na sheria za mtoto zinamlinda ipasavyo.

Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu, Bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amesema serikali inafanya jitihada za kupeleka miradi elekezi vijijini kwa kushirikiana na halmashauri.

Kwa mujibu wa waziri Majaliwa, mahusiano hayo yanalenga kuboresha mahusiano ya familia na kuhakikisha mtoto anabaki akilelewa katika ngazi ya familia hata anapopoteza wazazi au kutelekezwa kwani kuachwa hovyo husabisha madhara makubwa kwa mtoto na jamii kwa ujumla.