Jumanne , 6th Oct , 2020

Kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani tarehe 11 mwezi huu wa Oktoba, wadau wa mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike wameitaka jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike ambavyo vinadaiwa kuongezeka hapa nchini.

Irene Ishengoma, Meneja Miradi Global Peace Foundation.

Wakiongea na EATV leo wadau hao kutoka shirika la Macho kwa jamii na Global Peace Foundation wamesema licha ya serikali kuonyesha jitihada za kukomesha vitendo hivyo lakini jamii nayo inapaswa kufahamu kwamba vitendo hivyo havikubaliki kwenye jamii

''Kuna kila sababu ya jamii kuonyesha ushirikiano wa kukemea vitendo hivyo lakini pia kuvitolea taarifa pale wanapoviona badala ya kuvikalia kimya'', amesema Irene Ishengoma kutoka shirika la Global peace Foundation

Ameongeza kuwa, familia inapaswa kuachana na dhana potofu na badala yake kusimamia suala la mtoto wa kike kuhakikisha anakwenda shule ikiwa ni haki yake ya msingi badala ya kuona kama kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza fedha