Jumatatu , 3rd Jul , 2023

Jaji Mstaafu January Msoffe, amewataka wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kutojihusisha na masuala ya ulevi na tabia nyingine zinazokinzana na maadili ya Kitanzania ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Jaji Mstaafu January Msoffe

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Iringa Jaji Msoffe, amesema elimu bila maadili ni kazi bure hivyo kila mwananfunzi kuepukana na vitendo visivyofaa ikiwemo ulevi na mapenzi ya jinsia moja. 

"Unaweza ukawa na Degree au Masters lakini kama huna maadili ni kazi bure ,hivyo nasisitiza wanafunzi kuzingatia hilo lakini pia na watumishi wa umma wazingatie hilo," amesema Jaji Msoffe

Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Iringa amekiri kwamba tatizo la maadili kwa vijana bado ni tatizo kubwa hivyo kinatumia wasaikolojia kuwatibu na kuwajenga vijana katikamaadili mema

"Hilo tatizo ni kubwa akionekana mtu ambaye yupo kinyume na maadili ya Kitanzania hapa chuoni tunatumia vitengo vyetu vya maadili wakiwemo wanasaikoloji kuwatibu maana mtu kujigeuza jinsia hilo ni tatizo la kisaikolojio," amesema Makamu Mkuu wa Chuo