Jumatatu , 4th Dec , 2023

Jeshi la Israel limesema linapanua operesheni yake ya ardhini katika  maeneo yote  ya Ukanda wa Gaza kufuatia kuanza tena kwa mapigano siku ya Ijumaa

Amri mpya Imetumwa leo asubuhi kwenye mitandao ya kwa watu kuhama maeneo 20 ya eneo la Palestina.

Vikosi vyake vimekuwa vikishinikiza kusini zaidi  huku kukiwa na onyo kutoka kwa makundi ya kibinadamu kwamba watu wa Gaza wanakimbia maeneo ya kukimbilia

Maafisa waandamizi wa Marekani awali walirudia maoni yao kwamba Israel ina haki ya kujilinda - lakini wakaongeza kuwa wanajeshi wake lazima wawalinde raia.

Wakati huo huo, mshauri wa waziri mkuu wa Israel ameiambia BBC kuwa nchi yake inafanya "juhudi kubwa" ili kuepuka vifo vya raia.

Shambulio la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7 liliuwa watu 1,200, huku wengine 240 wakitekwa nyara.

Tangu wakati huo, wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas inasema zaidi ya watu 15,500 wameuawa katika kampeni ya kulipiza kisasi ya Israel, wakiwemo watoto 6,000.