Alhamisi , 25th Sep , 2025

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, ametangaza mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi yake haina dhamira ya kuunda silaha za nyuklia huku zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanzishwa tena kwa vikwazo.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, ametangaza mbele ya hadhara ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi yake haina dhamira ya kutengeneza silaha za nyuklia huku zikiwa zimebaki siku chache kabla ya vikwazo vya kimataifa kuanzishwa tena dhidi ya taifa hilo kutokana na shughuli zake za nyuklia.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimechukua hatua ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambavyo vilikuwa vimesitishwa chini ya mkataba wa nyuklia wa 2015 ambao ulifikiwa na Marekani na kisha kuvunjwa na Rais wa Marekani Donald Trump. 

Vikwazo hivyo vinatazamiwa kuanza kutekelezwa siku ya Jumamosi. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi alikutana Jumanne na mawaziri wenzake wa Ulaya, ikionekana kama njia ya kuepusha vikwazo na kuendeleza mazungumzo.