Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Mh. Lazaro Nyalandu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kusafirisha watalii mkoani Kilimanjaro Zara, Bi Zainab Anselem amesema Ugonjwa huo umeathri kwa kiasi kikubwa sekta ya Utalii kutokana na Taarifa zaidi za kuenea kwa ugonjwa huo kwa nchi za Afrika na kuiomba serikali kusaidia kuwaelesha zaidi watalii kuhusu Afrika.
Kwa upande wake Balozi wa Heshima nchini Marekani Bw. Ahmed Issa akiwa ameongozana na wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kuangalia fursa za Uwekezaji hapana nchini amesema watu wanavutiwa na Tanzania kwa sasa hivyo wamefanya juhudi za kuweza kuja na wataalamu mbalimbali ili kuwekeza katika nyanja tofauti.
Wakati huo huo, wafanyabiashara na makampuni makubwa ya utalii duniani, watakutana jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, katika kongamano kubwa la utalii litakalofanyika kuanzia Oktoba Mosi hadi nne jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo linaloandaliwa na Bodi ya Utalii nchini, linajulikana kama Swahili International Tourism Expo ambapo kwa mara ya kwanza linafanyika hapa nchini badala ya Afrika Kusini ambako limekuwa likifanyika mwezi Mei kila mwaka.
Akizungumzia kuhusu kongamano hilo, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki amesema kuwa hiyo itakuwa fursa nzuri kwa ukuzaji wa biashara na sekta ya utalii nchini ambapo makampuni ya Kitanzania, yatapata fursa mbali mbali za kibiashara na makampuni kutoka nchi za Asia, Ulaya na Amerika.