Ijumaa , 13th Mar , 2015

Idadi ya Vifo katika ajali ya iliyotokea jana mjini mafinga Mkoani Iringa imeongezeka na kufikia watu 50 baada ya majeruhi wengine kufariki dunia jana huku majeruhi wakibaki 14.

Moja ya picha za ajali iliyotokea hivi karibuni Mkoani Iringa, katika Mji wa Mafinga

Akiongea na East Africa Radio Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amesema kuwa majeruhi wengine wanaendelea vizuri na pia ndugu wa marehemu wameshaanza kuzitambua maiti za ndugu zao na kuzichukua kwa ajili ya maziko huku maiti nyingine zikiwa bado haizijatambuliwa.

Bi. Masenza amesema kuwa tayari miili 17 ya marehemu waliokuwa Hosptali ya rufaa Mkoa wa Iringa imetambuliwa na kati ya hiiyo 14 imechukuliwa na marehemu 10 bado hawajatambulika.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika hospitali ya Mafinga marehemu 21 wametambuliwa na nane kati yao wamechukuliwa na wawili hawajatambuliwa.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia ameitaka serikali kuchukua hatua kwa kila aliyehusika na kutokea kwa ajali hiyo, huku akitaka ufanyike uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kutoruhusu malori kusafirisha mizigo katika barabara moja pamoja na mabasi ya abiria.

Aidha mbatia amesema ipo haja kwa serikali kuangalia upya mifumo yake kwa madereva wanaobainika kukiuka shria za barabarani na kunyang'anywa Leseni zao.

Na Chama cha Wananchi kupitia taarifa yake iliyosainiwa na kaimu katibu mkuu wa CUF, Shaweji Mkweto kimetuma salamu za pole na rambirambi kwa majeruhi wote wa ajali hiyo na wafiwa na kuongeza kuwa masikitiko yake juu ya serikali kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na ajali za mara kwa mara.