Jumatano , 27th Sep , 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mkoa wa Mara na kukuta hali mbaya katika uendeshaji wa hospitali hiyo kwa kukosa baadhi ya vitu muhimu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla amegundua hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kuimalisha sekta ya afya ya siku mbili wilayani Bunda Mkoani Mara na kusikitishwa na baadhi ya vitu alivyokutana navyo katika hospitali hiyo ya mkoa ikiwemo mpangilio mbaya wa usafi wa vyombo vya upasuaji, baadhi ya vyumba kutokuwa na taa huku vingine vikiwa ndivyo sivyo.

Mtazame hapa Dk. Kigwangalla anavyozungumza pindi alipofika hospitalini hapo.