Jumanne , 15th Jul , 2014

Asilimia 78 ya watu wenye albinism ya wagonjwa wa saratani ya ngozi nchini Tanzania wanaofika hospitali kwa matibabu hawapati huduma hiyo kwa wakati.

Mkurugenzi wa asasi ya kimataifa inayotetea haki kwa walamavu wa ngozi tawi la Tanzania Bi. Vicky Ntetema.

Hakli hiyo imedaiwa kuchangiwa na urasimu uliokithiri katika kliniki na hospitali za wilaya kabla ya kupewa rufaa ya kwenda hospitali kuu ikiwa ni pamoja na hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hayo yameelezwa hapo jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Under the Same Sun UTTS Tanzania, Bi. Vicky Ntetema wakati akieleza namna ambavyo Bi. Rukia Kasembe Michenga mwenye albinism jinsi alivyoathirika na kupelekea kupoteza uwezo wa kuona sababu ya saratani kutokana na urasimu aliofanyiwa tangu mwaka 1999 alipoanza kuhangaikia matibabu.

Naye Meneja Uendeshaji wa UTTS, Gamael Mboya amesema Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 watu wenye albinism nchini ni kati ya elfu kumi na kumi na tatu hivyo serikali iweke kampeni maalumu ya Kutoa matibabu mapema kwa watu wenye albinism hali itakayosaidia kuepukana na saratani ya ngozi kwa kupata matibabu mapema.

Kwa upande wake mmoja wa waathirika wa saratani hiyo Bi.Rukia Michenga amesema hajapewa matibabu stahiki katika hospitali ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na baadae jijini Dar es salaam katika hospitali ya saratani ya Ocean road ili kupata matibabu lakini hajapatiwa matibabu kutokana na kukosa fedha kwa miaka 15 huku akielezea namna ambavyo amekatishwa tamaa na madaktari.