
Umoja wa Mataifa ambao ndio mtoaji mkubwa wa misaada Gaza unasema kazi yake itakoma usiku wa leo ikiwa haitapata vifaa vipya.
Israel inasitisha usambazaji mpya wa mafuta katika Ukanda wa Gaza, lakini inashutumu Hamas kwa kuhifadhi mamia ya maelfu ya lita
Malori mengine manane ya misaada yaliyobeba chakula, maji na dawa yalivuka kutoka Misri na kuingia Gaza jana usiku - lakini mashirika yanasema angalau malori 100 kwa siku yanahitajika
Serikali ya Hamas katika Ukanda wa Gaza inasema watu 80 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya usiku kucha ya Israel.
Israel inasema ililenga miundombinu ya Hamas - ikiwemo vizuizi vya barabarani vinavyodaiwa kuwa vimewekwa kuwazuia raia wanaohama kutoka Ukanda wa Gaza kaskazini
Wizara ya afya ya Gaza imesema kuwa takriban watu 5,800 wameuawa tangu Oktoba 7 mwaka huu.
Zaidi ya watu 1,400 waliuawa katika mashambulizi ya awali dhidi ya Israel na kundi la Hamas, na zaidi ya watu 200 bado wanashikiliwa mateka.