Jumamosi , 10th Jul , 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi katika hili wimbi jipya la Corona kwani kasi ya wagonjwa imekuwa ikijitokeza na kulazwa katika hospitali.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima

Dkt Gwajima ameongeza kuwa serikali pia imekua ikifanya nguvu kubwa ili kuhakikisha watu fulani wanaongoja maafa fulani kwa nchi yatokee bali yasitokee na kuomba wananchi ambao hawaitikii maelekezo waitikie ili hali iendelee kuwa salama zaidi.

"Watanzania wachukue tahadhari hali ingawa imedhibitiwa lakini inaendelea kuja na kasi ya wagonjwa kuendelea kujitokeza na kulazwa, watu wasidhani kwamba tunasubiri hali iwe basi mtaani tunaziona maiti ndiyo tuanze kazi, kazi inayofanyika ni kuifanya hali isiwe mbaya na serikali imekuwa ikijitahidi, wagonjwa wapo na wanaendelea kujitokeza na maambukizi yanaendelea kujitokeza na hii sio uongo,” amesema Dkt Gwajima.