
Katibu Mkuu wa mkutano wa kimataifa kuhusu eneo la Maziwa Makuu, Zachary Muburi-Muita.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa mkutano wa kimataifa kuhusu eneo la Maziwa Makuu, Zachary Muburi-Muita alipozungumzia suala hilo Umoja wa Mataifa.
Balozi Muita amesema upande wa serikali na upinzani katika mataifa hayo ni lazima kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi.
Amesema, hali ya usalama inaimarika nchini Burundi na mchakato wa mazungumzo unaendelea Arusha,Tanzania, lakini hatima ya kisiasa bado iko njia panda.