Mbunge wa Kawe Halima Mdee, na CAG Prof Mussa Assad
Baada ya kuhojiwa kiongozi huyo, Januari 22 tena ilishuhudiwa Mbunge wa Kawe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee na yeye akihojiwa mbele ya Kamati hiyo juu ya kuunga mkono kauli iliyotolewa na CAG.
Hatma ya wawili hao sasa iko mikononi mwa Spika Job Ndugai baada kamati iliyowahoji kuwasilisha taarifa yao kwa kiongozi huyo wa Bunge, pamoja na kuweka mapendekezo ya nini kifanyike dhidi ya watu hao wawili.
Hii ni mara ya kwanza kushuhudia CAG akihojiwa na kamati ya Bunge lakini si mara ya kwanza kwa Mbunge wa Kawe kuhojiwa na kamati hiyo ambapo mwaka 2017 alihojiwa na na kamati hiyo na kufungiwa mwaka mmoja kutohudhuria vikao vya Bunge.
Katika hukumu hiyo Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Esther Bulaya walihukumiwa kwa kosa la kutotii mamlaka ya kiti cha Spika wakati alipoagiza kuondolewa nje kwa Mbunge wa Kibamba John Mnyika.