Banda la Kuku
Kwa mujibu wa Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Habtie Tekie amesema harufu inayotoka kwenye kuku inaweza kutumiwa na kutengeneza dawa itakayowafukuza kabisa wadudu hao hatari.
Jaribio lililofanywa na watafiti hao Magharibi mwa nchi ya Ethopia lilihusisha kuku aliewekwa chini ya kitanda katika eneo lenye mbu na mtu kulala chini ya kitanda hicho na alithibitisha kutong'atwa na mbu yoyote.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolwa na Umoja wa Mataifa, mwaka jana pekee jumla ya watu 400,000 Afrika wamefariki kwa ugonjwa wa Maralia pamoja na kwamba maambukizi na vifo hivyo vimeonyesha kupungua.
Matokeo ya utafiti huo yamebainisha kuwa mbu hufuata chakula chao kwa kupitia harufu lakini hawawezi kukaa eneo lolote ambalo lina harufu ya kuku kwa kuwa hawapatani nayo.