Haniu achukua nafasi ya Msigwa

Jumatano , 9th Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaffar Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, akichukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na msemaji mkuu wa serikali.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Jaffar Haniu

Kabla ya uteuzi huo Bw. Haniu alikuwa mtendaji wa vyombo vya habari vya Africa Media Group Limited, na uteuzi wake unaanza rasmi leo Juni 09, 2021.

Soma zaidi hapo chini