Jumanne , 28th Jul , 2015

Sakata la wabunge kuhama kutoka chama kwenda kingine limeendelea tena kwa wabunge wengine kuhama vyama vyao akiwemo Bi. Leticia Nyerere mbunge wa vitu maalumu kupitia CHADEMA kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Chadema Leticia Nyerere.

Akizugumza na Waandishi wa Habari jana Bi. Leticia amesisitiza kuwa uamuzi wake wa kuingia CHADEMA, ulikua wa kukurupuka hivyo ameamua kurudi CCM chama ambacho ni chama kilimlea tangu alipoanza siasa.

Leticia amesema kuwa amekaaa CHADEMA kwa kipindi cha miaka mitano lakini hakuna mafanikio aliyoyapata katika utendaji kazi wake zaidi ya kusononeka kwa kukosa vitu muhimu.

Wabunge wengine waliohama CHADEMA, ni Pamoja na Chiku Abwao wa Iringa Muhonga Luhanywa wa Kigoma na Marry Stella Malack ambao wote wamehamia chama cha ACT-Wazalendo.