Alhamisi , 26th Mei , 2016

Serikali imesema kuwa itachukua hatua kali kwa halmashauri yoyote nchini ambayo haitatenga asilimia 20 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji nchini.

Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene.

Akizungumza leo mjini Dodoma, Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene amesema kuwa halmashauri hazina budi kutenge fedha hizo kwa ajili ya viongozi hao ambao ni muhimu katika maendeleo ya halmshauri hizo.

Mhe. Simbachawene amesema itakua ni jambo la ajabu na kusikitisha endapo kuna halmashauri haionyeshi kuwajali viongozi hao ambao ni wasimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja ukusanyaji wa mapato ya Halmshauri.

Waziri huyo wa TAMISEMI amesema serikali itahakikisha kuwa mpango huo uliowekwa na serikali wa kutenga asilimia 20 kwa ajili ya viongozi hao unatekelezeka huku akiwata wabunge ambao nao ni moja ya wawakilishi katika halmshauri wasadie kufanikisha suala hilo.

Aidha, Mhe. Simbachawene amezitaka halmashauri kuweka vipaumbe kutokana na ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kujenga ofisi za watumishi hao wa Umma ili kuwawekea mazingira mazuri ya ufanyiakazi.

Sauti ya Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa,Mhe George Simbachawene