Jumatano , 6th Jan , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema watu waliojenga mabondeni wanaobomolewa nyumba zao hawatal

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema watu waliojenga mabondeni wanaobomolewa nyumba zao hawatalipwa fidia ikiwemo kupewa viwanja na kuonya kuacha kuvamia mashamba ya watu kwa kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkuu huyo wa Mkoa Bw, Meck Sadick amesema kuwa wakazi hao wa mambondeni wanapaswa kuondoka wenyewe wasisubiri fidia ambayo haipo.

Meck Sadick amesema hayo huku zoezi la Bomoa bomoa likiwa linaendelea katika maeneo ya Mkwajuni huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linafanywa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ambayo inawataka wananchi wasijenge katika maeneo hatarishi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa zoezi hilo sio la Dar es Salaam peke yake kama wengi wanavyodhani bali ni la nchi nzima na litaendelea kwa kadiri siku zinavyokwenda.