Jumatano , 13th Jul , 2016

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limewataka wananchi wa mkoa ambao bado hawajahakiki silaha zao wawasilishe silaha zao kwa hiyari kabala jeshi hilo halijaanza msako wa kuzitafuta kwa operesheni maalumu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata Mzinga.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani humo Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi Renata Mzinga, amesema jeshi la polisi lilikwishatoa muda wa kutosha kwa kila raia kwenda kuhakiki silaha anayomiliki hivyo kama kuna mtu anamiliki silaha ambayo haijakikiwa ni vyema aiwasilishe kwa hiyari yake.

Kamanda mzinga amesema kuwa kwa wale watakaokamaatwa katika operesheni hiyo watahesabiwa ni wale ambao wanakuwa na nia mbaya na silaha hizo hivyo jeshi litaangalia utaratibu wa kuzirejesha mikononi mwao.

Aidha Kamanda mzinga ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwafichua wato wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na jeshi hilo litaweza kumaliza tatizo la umiliki wa silaha kiholela endapo tu wananchi watatoa ushirikiano kwa jeshi hilo.