
Naibu Spika ameyasema hayo kufuatia wabunge wa upinzani kwa siku kadhaa sasa kususia vikao vya Bunge kwa kusaini mahudhurio na baada ya kuanza kwa vikao kutoka nje ya ukumbi kwa kutokuwa na imani na naibu spika wa Bunge.
Naibu Spika ameyasema hayo baada ya kuombwa miongozo na wabunge wawili akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe juu ya wabunge wa upinzani kususia vikao.
‘’Sii sahihi wala halali kwa Mbunge kupokea posho bila kufanya kazi kitendo cha kujisajili na kutoka ukumbini hakikubaliki kuna haja ya kuangalia namna ya kurekebisha sheria ili wabunge walipwe kulingana na kazi wanazofanya’’-Amesema Naibu Spika.
Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Peter Msigwa amesema si lazima Mbunge aingie ndani ya Bunge kila siku, kufanya kazi za kibunge mtu anaweza kuwepo kwenye vikao vinavyohusu kuwawakilisha wananchi na jambo hilo linaruhusiwa na kanuni.