Viongozi wa Jumuiya hiyo wamekutana huko New York ambapo wanahudhuria mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa.
Wamekubaliana kuwawekea vikwazo idadi ya watu ambao idadi ya majina yao itatajwa muda wowote. Viongozi wa kijeshi nchini Guinea wamesema kwamba wanahitaji miaka mitatu ili kuiweka nchi hiyo sawa kidemokrasia na kwamba hawaridhishwi na matakwa ya Ecowas ya kutaka mabadiliko hayo yafanyike haraka iwezekanavyo.
Guinea imeondolewa kwenye umoja wa Ecowas kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea mwezi Septemba mwaka jana.