
Ofisi ya kampuni ya Google iliyoko London Uingereza
Ujio wa habari hiyo ni mafanikio makubwa kwa sekta ya teknoloJia nchini Uingereza.
Mkurugenzi mtendaji wa Google, Sundar Pichai, ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kuwa Uingereza bado ni sehemu sahihi kwa uwekezaji.
Amesema kufungua kwa mipaka na uingiaji huru kwa wahamiaji wenye ujuzi ni suala muhimu kwa mafanikio ya tekinolojia nchini Uingereza.