Jumatatu , 12th Aug , 2024

Dereva bodaboda aitwaye Kabichi John, amefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Nadia kukosa mwelekeo na kuwagonga  wakiwa pembezoni mwa barabara katika eneo la Buhare Manispaa ya Musoma huku gari hiyo ikiteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali.

Gari lililochomwa moto

Wakizungumzia tukio hilo la ajali baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema tukio hilo limetokea baada ya gari hiyo kukosa mwelekeo na kuwagonga watu hao ambao walikuwa pembezoni mwa barabara huku wakidai kuwa gari hiyo ilikosa mwelekeo kutokana na dereva kuendesha kwa kasi akisadikiwa alikuwa amegonga katika eneo lingine na hapo alikuwa anakimbia.