.jpg?itok=u--YDcpr×tamp=1475487232)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
Wito huo umetolewa na baadhi ya wazee walioshiriki mafunzo ya usalama barabarani, ujasiriamali pamoja na ulinzi shirikishi iliyohusisha zaidi ya watu 160 wakiwemo madereva bodaboda.
Wakizungumza kwenye mafunzo hayo wazee hao wamelishukuru shirika la Apec kwa kushirikiana na jeshi la polisi kutoa mafunzo kwa madereva bodaboda hao ili waweze kuona faida na matunda ya kazi wanayoifanya.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru, Nyangusi Nailiba, akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo amemwagiza Mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha madereva bodaboda wote wanaweza kupata mafunzo ili waweze kufanya kazi zao kwa salama.