Alhamisi , 9th Jan , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kupitia upya na kama itawezekana, kuvunja mkataba wa ujenzi wa moja ya barabara iliyopo ndani ya hifadhi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Mrisho Gambo amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa kuwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kushindwa kutekeleza kwa viwango na muda aliopewa.

Gambo amesema haridhishwi hata kidogo na utendaji kazi wa mkandarasi huyo, ambaye ni mzawa, ambapo kati ya Kilometa 78 ni Kilometa 14 tu ambazo ameashaanza kutengeneza huku barabara hiyo, yenye urefu wa kilometa 78, inayotokea  eneo la View Point kuelekea Kijiji cha Nayobi ndani ya hifadhi hiyo imetajwa kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.3, huku zikiwa zimelipwa Mil 200.