Alhamisi , 17th Oct , 2024

Hali ya Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua imeelezwa kuwa tete baada ya kukumbwa na maumivu makali ya kifua hali iliyopelekea kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Kauli juu ya taarifa ya ugonjwa wa Gachagua imetolewa jioni ya leo Oktoba 17, 2024 na Wakili wake Paul Muite, hii ni baada ya Naibu Rais huyo kushindwa kufika kwenye Bunge la Seneti kwa ajili ya kujitetea kufuatia mashtaka 11 yaliyowasilishwa dhidi yake.

Ikumbukwe kuwa siku ya leo Bunge la Seneti lilikuwa limsikilize Gachagua na kumpa nafasi ya kujitetea kabla ya kutoa uamuzi kwa njia ya kura ambapo kati ya maseneta 67, 45 kati yao wanahitajika kupiga kura kuunga mkono Muswada ili kumuondoa Gachagua madarakani na iwapo idadi ya maseneta watakaounga mkono Muswada huo haitafika 45, Gachagua atakuwa huru kuendelea na majukumu yake.