Ijumaa , 23rd Sep , 2022

Mbuzi 10 wamekufa na wengine 9 kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na kundi la Fisi usiku wa kuamkia leo Septemba 23, 2022, kwenye zizi la Masunbuko Shirungu mkazi wa Kijiji cha Itale wilayani Chato mkoani Geita na baadae Fisi huyo aliuawa na Mbwa wa mfugaji.

Mbuzi waliokufa kwa kushambuliwa na Fisi

Afisa Mifugo na Uvuvi wilaya Chato Dokta Elfas Msenya, ameeleza hasara iliyojitokeza kwa nfugaji huyo.

"Mbuzi 1 kwa sasa wastani wa bei ni shilingi  90,000 zidisha mara idadi ya mifugo iliyoathirika utaona hasara ilivyokubwa", amesema Msenya.

Aidha Msenya anaelezea hatua za awali walizochukua kuhakikisha mifugo minginge haikumbani cha changamoto ya kuliwa na Fisi.

"Hatua za haraka tukizochukua kwa sasa, tumewashauri kuimarisha mabanda yao au wajenge mabanda imara bila kusahau kuimarisha ulinzi hasa nyakati za usiku lakini pia kutowafuata wanyama wakali kwenye makazi yao na waache kujenga karibu na maeneo ya mapori,".