Rais Samia wakti akirekodi filamu hiyo
Naibu Waziri Masanja ameyasema hayo leo Julai 11,2023 alipotembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea Jijini humo.
"Tunatambua kwamba ni nadra sana kumpata kiongozi anayeamua kuongoza kwa vitendo kama alivyofanya Rais Samia, ametangaza kwa vitendo vivutio vyetu hivyo tunatakiwa kuvitembelea vivutio hivyo ili kumuunga mkono," amesema
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini akitolea mfano wa maeneo ya Malikale, Misitu ya Asili, tamaduni za Kitanzania, historia za Tanzania za Waasisi wa Taifa na maeneo mengine ya utalii.