
Mkuu wa Idara ya Viwanda na ushindani wa Jumuiya ya SADC, Johansein Rutaihwa.
''Tanzania inakwenda sambamba na SADC kwa kuweka nguvu kwenye viwanda na sisi kama Jumuiya tunahakikisha tunawasaidia kufikia malengo hayo na sio kwa Tanzania tu ni nchi zote wanachama'', - @johansein#EABreakfast
— East Africa Radio (@earadiofm) August 8, 2019
Rutaihwa ameyabainisha hayo leo kupitia East Africa Breakfast ya East Africa Radio, ambapo ameeleza mipango pamoja na utendaji kazi wa Jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake.
''Jumuiya ya SADC tumejiwekea malengo kwa kila mwaka kila nchi mwanachama wa SADC uchumi ukue kwa asilimia 7 kuanzia mwaka 2016ambapo Tanzania pekee ilifikia lengo, ikifuatia na DRC ambao uchumi wao ulikuwa kwa asilimia 6.3 na Angola kwa asilimia 5.7'' - @johansein#EABreakfast pic.twitter.com/ul5be5ykRs
— East Africa Radio (@earadiofm) August 8, 2019
Kwa upande mwingine Rutaihwa ameeleza kuwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika inafanyakazi kwa ukaribu na Jumuiya nyingine ili kuhakikisha kwa pamoja bara la Afrika linapiga hatua.
''SADC tunafanyakazi na Jumuiya zingine kama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) pamoja na Jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ili kuhakikisha hakuna vikwazo kati ya nchi na nchi'' - @johansein#EABreakfast pic.twitter.com/dkNmID1qts
— East Africa Radio (@earadiofm) August 8, 2019
Aidha amebainisha kuwa katika kuelekea mkutano huo wa wakuu wa nchi hizo ambao utafanyika Agosti 17-18 mwaka huu, lakini shughuli mbalimbali ikiwemo maonyesho ya biashara na viwanda kwa nchi wanachama yanaendelea.
''Kabla ya kuanza maonyeshao ya SADC, kulikuwa na watu 2800 ambao walikuwa wamejiandikisha lakini kuna wengine, waliongezeka na kuwa zaidi 3000 wakiwemo wageni kutoka nchi wanachama wa SADC'' - @johansein - Mkuu wa Idara ya Viwanda na ushindani SADC.#EABreakfast
— East Africa Radio (@earadiofm) August 8, 2019