Jumanne , 20th Oct , 2015

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji (EWURA) imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa mafuta atakaetengeneza uwepo wa upungufu wa mafuta katika kipindi hiki cha kampeni.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa nishati,maji nchini Felix Ngalamgosi.

Akiongea jana Jijini Dar es Slaam Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi katika kikao cha kutathmini hali ya mafuta kuelekea uchaguzi amesema ni wajibu wa wafanyabiashara wa mafuta kufata sheria za leseni zao na kusaidia uzalendo wa nchi na atakae kiuka atafungiwa.

Tayari EWURA imeshazifutia leseni kampuni nae za Biashara ya mafuta kutokana na kukiuka masharti ya leseni za kufanyabiashara ya Petroli ambao walionekana kwa makusudi kusababisha uhaba wa mafuta nchini.

Aidha Ngamlagosi aliuhakikishia umma kuwa yapo mafuta ya kutosha ambapo mafuta ya ndege jet A1, yapo ya siku 58, Petroli ya siku 27 mafuta ya taa ya siku 50, mafuta ya dizeli siku 15 na mafuta mazito ya mitambo ya siku 89 huku meli zingine zinaendelea kuingiza mafuta mengine.