Taarifa zilizotolewa na Meneja wa Maudhui wa Clouds Media Group, Sebastian Maganga, zinasema kwamba wanasubiri taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kuweza kupata taarifa zaidi juu ya kifo cha mtangazaji Ephraim Kibonde.
Sebastian Maganga amesema kwamba msiba upo nyumbani kwa marehemu Ephraim Kibonde Mbezi chini mkabala na Safari resorts Hotel, na mwili unatarajiwa kuwasili usiku wa leo saa 4, na utaenda kuhifadhiwa Hospitali ya Lugalo, huku ukitarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi ya Machi 9, katika makaburi ya Kinondoni.
Ephraim Kibonde alianza kuugua akiwa mkoani Kagera, ambako walienda kwenye mazishi ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba na baadaye kukimbizwa mkoani Mwanza na kufikwa na umauti.
