
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga amemuagiza Mkandarasi anayejenga Barabaraya Dodoma –Mayamaya yenye urefu wa Kilomita 43.65 kumalizia kipande cha barabara ya kutoka Dodoma hadi Msalato yenye urefu wa KM 8 ifikapo Oktoba mwaka huu.
Eng Nyamhga ametoa agizo hilo mkoani Dodoma alipokuwa akikagua ujenzi wa wa barabara ya Dodoma Mayamaya yenye urefu wa kilomita 43.65 Mayamaya-Mela na Mela -Bonga km 188.15 ambapo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.
Aidha Eng Nyamhanga amewataka makandarasi wanaoendelea na miradi ya ujenzi wa barabara nchini kuongeza kasi ya ujenzi ili waweze kukamilisha ujenzi wa barabara hizo kwa wakati ili zitumike kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye Mkandarasi wa kampuni ya Sinohydro Coropration anayejenga sehemu ya barabara ya Dodoma Mayamaya yenye urefu wa(KM 43.65) Eng. Zeng Yun amemuhakikishia Katibu mkuu huyo kuwa ujenzi wa Barabara hiyo utakamilika kwa wakati uliopangwa.
Barabaraya Dodoma –Mayamaya,Mayamaya –Mela-Bonga yenye urefu wa(KM 188.15) ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The great North Road) kutoka Iringa kwenda Arusha kupitia Mikoaya Dodoma na Manyara