Ijumaa , 8th Jul , 2016

Mkoa wa Songwe unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 2621,vyoo pamoja na nyumba za walimu 4185 kati ya zinahitajika mkaoni humu huku wakiwa bado hajakamilisha tatizo la ukosefu wa madawati kama agizo la rais linavyotaka.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni Chiku Galawa.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani huo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu Chiku Galawa, ameongeza siku siku hadi Julai 25 kukamilisha madawati katika wilaya zote huku akisema mkoa umeanza mipango ya kutatua matatizo ya madarasa na nyumba hizo za walimu.

Mkuu wa mkoa huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa mkoa unahitiaji nyumba za walimu zaidi ya elfu saba mdarasa elfu 600 na matundu ya vyoo zaidi ya 9500 ambapo amesema baadhi ya maeneo utekelezaji wa kutatua changamoto hizo umeanza.

Amesema changamoto ya Madarasa imezidi kuongezeka mkoani humo kutokana na sera ya sasa ya elimu bure hivyo katika kuweka mazingira bora ya elimu wazazi na walezi pamoja na jamii kwa ujumla hawana budi kuchangia juhudi za serikali kuweka mazingira safi ya elimu.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Mkoa amesitisha vibali voyote vinyatolewa kwa ajili ya uvunaji wa misitu ya mbao mkoani humo kutokana na uharibifu wa mazingira na endapo mtu atakamatwa na mbao zitataifishwa na kutengenezea madawati kama Waziri Mkuu alivyoagiza.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni Chiku Galawa,