Jumanne , 29th Apr , 2014

Serikali ya Tanzania imesema kuwa sekta ya elimu ni mojawapo ya sekta sita zilizohusishwa katika mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN), ikifuatiwa na Maji, Nishati, Fedha, Kilimo na Usafirishaji.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Kassim Majaliwa

Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa - Tamisemi Mh. Kassim Majaliwa amesema mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) umeandaa vigezo vya kuinua kiwango cha ubora wa elimu kwa kuweka malengo ya viwango vya ufaulu vitakavyofikiwa mwaka 2014 ambavyo ni asilimia 70 na mwaka 2015 ni asilimia 80.

Aidha Mh. Majaliwa amesema utekelezaji wa mikakati yampango wa matokeo makubwa sasa upo katika hatua mbalimbali na unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya ofisi ya waziri mkuu Tamisemi na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambapo maadhimisho ya juma la elimu ni matokeo ya utekelezaji wa mkakati wa kutoa
tuzo kwa shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya darasa la saba na kidato cha nne 2013 ili kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katika kutoa elimu bora.