Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Thomas Mapuli amesema mashamba hayo yameteketezwa katika operesheni iliyoendelea mkoani humo yenye lengo la kuwabaini watu wote wanahotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Aidha Kamanda Mapuli amesema Jeshi la Polisi litaendelea kufanya Operesheni za mara kwa mara ili kukomesha biashara hizo haramu huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kutoa taarifa za watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.