Jumatano , 30th Apr , 2014

Jumuiya ya Afrika Mashari imesema itahakikisha inapambana na vita dhidi ya ugaidi katika nchi wananchama wa jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais uhuru Kenyata

Mwenyekiti  wa  wakuu  wa  nchi za  Jumuiya ya  Afrika  Mashariki Rais  Uhuru Kenyetta wa  kenya  amesema nchi   wanachama wa  jumuiya  hiyo  zitahakikisha   vita dhidi  ya ugaidi  inaendelea  kuimarishwa  na  kuhakikisha  wananchi   wake wanaishi  kwa  amani.

Mh  Rais  Uhuru  Kenyata  amesema  hayo  baada  kumalizika  kwa kikao  cha  ndani   cha  marais  wa nchi  za  Jumuiya  hiyo ambacho  nchi  ya  Rwanda  iliwakilishwa  na  waziri  mkuu  na Burundi  iliwakilishwa  na  makamu  wa  kwanza  wa Rais.
 
Kuhusu   hatima   ya  sudani  kusini  kujiunga katika   jumuiya  hiyo    rais   kenyata   amesema   jitihada   zinaendelea   za  kuhakikisha   kuwa   amani    inapatikana   kwanza   katika   nchi  hizo na   ameendelea   kuwataka   viongozi   kutimiza   makubaliano  yao   yaliyowekwa   hapo  awali  yakiwemo  ya  kusimamisha mapigano.

Aidha  wakuu  hao  wa  nchi  za  Jumuiya  ya  Afika  Mashariki  pia walishuhudia  kuapishwa   kwa   majaji    watatu   wa   mahakama  ya   jumuiya     sambamba   na   kuzinduliwa   kwa mtandao  wa   kuwawezesha  wananchi  wa  nchi  hizo  kufungua  kesi   mahali popote  walipo   bila  kufika  mahakamani.

Hatua hiyo imemgusa   msajili   wa  mahakama hiyo   Prf   John   Ruhangisa ambaye  amesema kuwa itapunguza  changamoto nyingi  zilizokuwa zinawakabili
 katibu   mkuu wa  Jumuiya hiyo   Dkt.  Richard  Sezbera  amesema  baada  ya kukamilika   kwa   mkutano huo  baada  ya kupokea   mapendekezo  mbalimbali   ya  baraza   la   mawaziri   hatua  inayoifuata ni maandalizi  ya  katiba ya  ya  shirikisho.