Ijumaa , 4th Aug , 2023

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson, amewataka Wananchi hususani vijana kutumia fursa ya uwekezaji katika kilimo ili kujitengenezea ajira ya kudumu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 4 Agosti, 2023 wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (NaneNane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

"Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuwekeza na kuwawezesha vijana kujikita katika kilimo ikiwemo uanzishwaji wa mradi wa mashamba makubwa ya kuwezesha vijana kulima kibiashara (BBT) hivyo basi hakuna budi kila mmoja kuona ipo tija ya kushiriki katika uwekezaji huu," amesema Dkt Tulia

Ameongeza kuwa ni wajibu wa kila Mwananchi kuungana na serikali katika kutimiza azma ya kufanikisha mapinduzi ya kilimo nchini yanazaa matokeo chanya.