
Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada Takatifu, Kanisa Katoliki Njombe
Mhe. Dkt. Philip Mpango ameyasema hayo leo Aprili 3, 2022 aliposhiriki Ibada ya Misa Takatifu ya domonika ya tano ya Kwaresma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yoseph, Jimbo Kuu Katoliki la Njombe, ibada ilioongozwa na Mhashamu Askofu John Ndimbo.
Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa utunzaji na usafi wa mazingira na kuwahimiza kuendelea kulinda na kutunza mazingira mazuri yanaowazunguka.
Kwa upande wake Mhashamu Askofu John Ndimbo amemshukuru Makamu wa Rais kwa kushiriki ibada hiyo na kumuhakikishia kwamba kanisa Katoliki kwa miaka mitatu limetoa kipaumbele cha pekee katika uhifadhi wa mazingira kwa kuzingatia umuhimu wake kwa maendeleo endelevu.