Jumatano , 20th Apr , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli, amwataka waandishi na Wahariri wa Vyombo vya habari nchini kuwa wazalendo wa kuitangaza Tanzania katika vyombo vyao ili rasimali zake zitambulike kimataifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni ambalo litakua mfano Afrika mashariki, huku akiwaomba kutoa andika pekee bila kuijali nchi kwanza.

Dkt. Magufuli amesema kuwa kama waandishi wasipoitangaza Tanzania hakuna mwingine wa kuweza kufanya hivyo na ndio maana hata nchi jirani wanadiriki kunadi maliasili za Tanzania kuwa zinapatikana nchini kwao.

Aidha rais Magufuli amewaomba wahariri wa habari kuweka kurasa za mbele habari za maendeleo pia sio kila baya ndio ziwe katika ukurasa wa mbele bila kujali mazuri yaliyofanyika kwa wakati huo.

“Kwa ndugu zangu waandishi ninawaomba muitangaze Tanzania, muitangaze Tanzania mmuipende Tanzania, tusiwe wepesi wa kuandika mabaya tu ya Tanzania kila baya lipo kwenye front page zuri hakuna”Rais Magufuli alisema

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli.