Ijumaa , 11th Dec , 2015

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amesema lengo la serikali yake kupunguza bazara la mawaziri ni kuwataka mawaziri walioteuliwa wafanye kazi,

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli

Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa hakutakuwa na semina elekezi ambapo ameagiza fedha zaidi ya shilingi bilioni 2 zilizotengwa kwa semina hiyo kuchukuliwa na kutumika katika shughuli nyingine.

Akiongea mara baada ya kutangaza baraza la mawaziri jana Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais Dkt. Magufuli amesema fedha hizo zitaelekezwa katika maeneo mengine ya kama vile kununua madawati na kusaidia sekta ya elimu lakini pia watakaa na kupanga vizuri sehemu ya kuzielekeza fedha hizo.

Aidha Dkt. Magufuli amesema serikali imeokoa mabilioni ya shilingi kutokana na kuchelewa kwa kutangaza baraza la mawaziri lakini pia kupunguza wizara ambapo wafanyakazi wengine watapungua kutokana na kupungua huko na kusema fedha hizo itaenda kusaidia kutatua kero za Watanzania.

Aidha, Dk. Magufuli akatuma salamu kwa mawaziri aliowateuwa katika baraza lake ambao wanapenda kufanya sherehe wajue wamepewa kazi ngumu na iwapo watafanya sherehe hizo wajiandae na kufanya sherehe pia wakati watakapotimuliwa kazi.