Waziri Dorothy Gwajima
Ameyajibu hayo katika mtandao wa X ambao alipokea malalamiko kutoka kwa moja ya mwananchi aliyelalamika kutokupewa ushirikiano na wizara yake pamoja na Wizara ya Afya kwa msaada wa matibabu kwa mtoto aliyezidiwa na wazazi wake walihitaji msaada wa matibabu.
“Hebu twendeni taratibu kwa utaratibu tafadhali. Kila wizara inao utaratibu wake mahsusi kwa mawasiliano na jamii kwa taarifa mbalimbali. Wizara zote zimetangaza namba zao ikiwemo afya, tamisemi, Katiba na Sheria, mambo ya ndani nk. Hivi, ukija na hoja yako ukapewa mwongozo kuwa, tafadhali fanya hivi, nalo kosa? kama umepiga hawajapokea wakati huo, namba hizo zinaruhusu na kutuma ujumbe wa kuandika, je unakuwa umefanya hivyo? Haya, hatua ingine, wizara zote ziko online na unaweza kutuma DM na ukawa-Tag, nayo hiyo imeshindikana? nadhani ni vema kutendeana kwa haki.” Ameandika Dkt. Ngwajima