Jumatano , 21st Aug , 2024

Mahakama ya wilaya ya Ruangwa imemhukumu Juma Saidi Selemani almaarufu kama Dj Mushizo (23) mkazi wa Kijiji cha Nandanga wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwenda jela kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto Salma Nurdin Hussein mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo ya kesi ya Jinai namba 3071/2024 imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa Yasinta Kingwala mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mkaguzi wa Polisi Bocho Matiko baada ya mtuhumiwa huyo kukutwa na hatia. 

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 10, 2024 na kukamatwa Januari 11, 2024 kisha kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka lake lililokuwa linamkabili lakini mtuhumiwa alikana kosa uUshahidi ulimtia hatiani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.