Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake amesema amekuwa diwani mwaminifu kupitia chama hicho kwa miaka mitano iliyomalizika mwaka huu lakini alikuwa akipishana kauli na viongozi wa chama hicho kuendeleza unyonyaji kwa wananchi.
Amesema sera mbovu za chama hicho ndiyo sababu ya wilaya ya Kyela kutokuwa na maendeleo kutokana na viongozi waliopo kuendekeza ufisadi wa kutaka kujinufaisha wenyewe na familia zao na kuwaacha wananchi wakiwa hawana wa kuwasemea matatizo yao.
Kinana ambaye ambaye mwaka 2010 alichaguliwa kwa kura nyingi kupitia chama hicho, alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wiki iliyopita na kupokelewa kwa kishindo na viongozi wa CHADEMA na kusema siku ya Jumamosi wakati wa kutambulishwa na chama atatoa yamoyoni.
Katibu wa siasa itikadi na uenezi wa CCM Richard Kilumbo amesema chama chake kilipanga kumuengua diwani huyo kutokana na makosa mengi aliyoyafanya ikiwemo zoezi la mbolea za ruzuku wakati akiwa diwani na kuwa kitendo chake cha kuhama ni kama amewahi kabla wao kufanya maamuzi.