Jumanne , 24th Jan , 2023

Diwani wa kata ya Agondi Halmashauri ya Itigi mkoani Singida  Emmanuel Soghweda amepiga marufuku wanafunzi kupanda malori wanaporudi nyumbani kutoka shule hali ambayo inaweza kuleta madhara ya kukatisha masomo kwa kupata ujauzito na maradhi,

Imeelezwa kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanafunzi hususani wa kike katika shule ya msingi Kamenyanga kata ya Agondi halmashauri ya Itigi mkoani Singida kupanda malori mara baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani

Shule hii ya Sekondari Kamenyanga ni miongoni mwa shule ambazo zipo jirani na barabara kuu ya Dodoma - Singida

William Njema ni afisa elimu kata na Nuru Maulid wanakiri kuwepo kwa tabia hiyo na mara kadhaa wamekuwa wakichukua hatua ya kuwashusha katika malori huku changamoto kubwa ikiwa ni kutembea umbari mrefu.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo ya sekondari Kamenyanga na mmoja wa wazazi wanaiomba serikali kujengewa mabweni ili kuondoa changamoto hiyo