Ijumaa , 9th Jun , 2023

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile, amewashukia wanasiasa wanaotaka kuwagawa Watanzania wanapojadili suala la makubaliano ya ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari kadhaa nchini ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma

Ditopile amesema, miaka miwili ya utawala wa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, umeonesha mafanikio makubwa kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Mbunge huyo amesema hayo kipindi ambacho kuna mjadala unaendelea wa ushirikiano huo kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ambapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiujadili kwa misingi wa u-Tanzania Bara na Uzanzibar.