Alhamisi , 17th Oct , 2024

Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Rebeca Nsemwa ameagiza Taasisi ya Kuzia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kuwachunguza msaidizi wa kituo cha afya Bahi pamoja na polisi kata Chipanga kuhusu utatata uliojitokeza kifo cha mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Lucia

Akizungumza na wananchi wa kata Chipanga mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema juu ya utata wa kifo hicho ambapo Lucia alikutwa amejinyonga, mkuu wa wilaya amesema wananchi wamekuwa wakificha matukio ya unyanyasaji kitendo ambacho kinahatarisha haki ya mtu ya kuishi katika jamiii.

“Chipanga mmenikwaza sana uhai wa mtu ni kitu muhimu sana na siwezi kufumbia macho matukio kama haya. Jeshi la poliosi kila siku linapigiwa kelele kwa sababu ya watumishi wasio waadilifu ndio kama huyo Masunga. Mkuu watakukuru naomba uwachunguze masunga na mtaalamu wetu wa kituo cha afya kwa sabau hawajafata taratibu katika kifo hiki matokeo yake inaonekana wamesaidia kuficha ushahidi.” Amesema mkuu wa wilaya Rebecca Nsemwa

Aidha wananchi wamemlalamikia mkuu wa wilaya kwa kukithiri kwa vitendo vya kupokea rushwa vya polisi kata ambae ametajwa kwa jina moja la Masunga ambavyo vinapelekea wananchi kutoripoti matukio ya unyanyasaji kwani mkuu huyo wa kituo cha polisi kata amekuwa akipokea rushwa kutoka kwa watuhumiwa na kumaliza kesi kienyeji.

“masunga ananyanyasa watu, masunga anachukua rushwa na ni mtu ambae kiukweli anaogopeka sana hapa ni mtu ambae mtu akiskia unapekekwa kwake unaogopa kutoka na anavyopokea rushwa” ameesema mwananchi.  

 

Sambamba na hilo mkuu wa wilaya amesema nalaani vitendo vya unyanyasaji ambavyo vimekuwa vikifanyika ikiwepo vitendo ambavyo alikuwa akifanyiwa Lucia kwa muda mrefu vilivyopelekea ujauzito wake kutoka huku akiwatupia lawama wanchi wa kata ya chipanga kwa kufumbia macho vitendo hivyo vilivyopelekea mama huyo kujitoa uhai.