Jumatano , 7th Oct , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewataka wasimamizi wa uchaguzi na jeshi la polisi kutenda haki siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu kwa vyama vyote.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva katika mkutano wa pamoja kati ya NEC na wasimamizi wa uchaguzi nchi nzima pamoja na Jeshi la polisi na kuongeza kuwa kama watendaji hao wakitenda haki na haki ikaonekana kutendeka basi Uchaguzi utakuwa huru na haki na hivyo kudumisha Amani na kuiepusha nchi na machafuko.

Kwa upande wa mkurugenzi msaidizi wa uchaguzi wa NEC Emmanuel Kawishe amesema makosa yote ya kiufundi yaliyotokea wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa BVR yanafanyiwa kazi pamoja na kuhakiki majina yote ili kutoa daftari lililokamilika siku 8 kabla ya Uchaguzi.

Kawishe ameongeza kuwa watu ambao vitambulisho vyao vimepotea hawatapiga kura na kila mtu atapiga kura pale tu alipojiandikisha.