Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Jackson Midala
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Jackson Midala amesema hayo leo katika mahojiano na EATV ambapo ametaja maeneo ambayo bado yanakosa huduma ya maji kuwa ni yale yanayohudumiwa na mitambo ya Ruvu juu ambayo ni pamoja na Tabata, Kimara, Mlandizi na Kibaha.
Midala amesema mafundi wa shirika hilo wanaendelea na ukarabati ili kuhakikisha maeneo hayo yaanza kupata huduma hiyo hii leo.